HAWA NDIO WANAOLALAMIKIWA KUENDELEZA HALI MBAYA ZA WAGONJWA MAHOSPITALINI!!

Mgomo wa madaktari ulianza kama utani vile, pale madaktari kadhaa walipositishiwa ajira zao katika hospitali ya taifa Muhimbili, ambapo baadae Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii alitoa kauli nzito iliyosababisha madaktari wengine nao kuanzisha mgomo.


Baada ya vuta nikuvute kati ya serikali na madaktari, huku wagonjwa wakiendelea kufa, Waziri Mkuu Mizengo Pinda akatoa tena kauli ambayo wengi walionyesha kutoifurahia, akisisitiza kuwa daktari ambaye hatarejea katika sehemu yake ya kazi, atakuwa amejifukuzisha kazi mwenyewe. Pamoja na kauli yake, madaktari hawakurudi. Baada ya madaktari kuendelea kugoma, wauguzi nao wakafuata, hali ndo ikazidi kuwa mbaya kabisa!


Spika wa bunge Bi. Anne Makinda, majuzi alikataa kulizungumzia suala hilo kama hoja ya dharura bungeni, kulikopelekea wananchi kushangazwa na hali hiyo.



 Jana kuna kipindi kilionyeshwa Channel Ten, na kwa waliotazama, kuna maoni mengi tu yalitolewa kupitia simu za watazamaji, wakiwataka viongozi hao hapo juu pamoja na rais Kikwete kulitafutia ufumbuzi ama kujiuzulu kwa kuwa limeonokana kuchukua sura nyingine kabisa! Wengine walimtaka rais Kikwete kuzungumzia suala hilo kwa kuwa toka lianze, hajawahi kutoa kauli yoyote.



Hali ni mbaya mahospitalini, hasa Muhimbili ambayo hupokea wagonjwa au magonjwa makubwa toka katika hospitali nyingine.
Mungu atusaidie tu kwa kweli manake tuliowapa dhamana ya kutuwakilisha katika uongozi ndo hao hao wagumu kutafuta ufumbuzi wa haraka ili tabu ziishe. Natoa pole kwa wagonjwa kwa kipindi hiki kigumu!

Comments