BREAKING NEWWWWWS....

WAANDISHI wa habari wawili na afisa wa uhamiaji Wilaya ya Handeni Mkoa wa Tanga wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya gari lao kupasuka gurudumu la nyuma upande wa kushoto na kupinduka.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Kostantine Massawe amewaambia waandishi wa habari kuwa tukio hilo limetokea majira ya saa 10:30 za asubuhi katika kijiji cha kwa maraha Wilayani humo.
Kamanda Massawe amewajata waliofariki dunia kuwa ni Mwandishi wa gazeti la Mwananchi communication Hussein Semdoe,Mwandishi wa gazeti la Uhuru na Mzalendo pamoja na Mariam Hassan ambaye ni afisa wa uhamiaji katika Wilaya hiyo.
Akielezea ajali hiyo Kamanda Massawe alisema gari hilo lilikuwa likitokea mjini Handeni na lilipata ajali katika eneo hilo wakati wakiwa katika ziara ya Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya hiyo.
Aidha Kamanda Massawe aliwataja waliojeruhiwa kuwa ni dereva wa gari hilo,Mtawala Makata,Mloi Napelion Afisa wa Maliasili wa Wilaya hiyo pamoja na Mshauri wa Mgambo wa Wilaya hiyo Constebol Atanasi Paulo.
Akizungumzia msiba huo, Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Tanga(TPC)Hassan Hashinu amesema msiba huo ni pigo kwa waandishi wa habari na mchango wao pamoja na jamii kwa ujumla haitausahamu.
“Wenzetu wametutoka mchango wao tutaendelea kuukumbuka katika ujenzi wa Taifa hili,”alisema Mwenyekiti huyo wa waandishi wa habari Mkoa wa Tanga.
Marehemu Semdoe na mwenzake Hamisi Bwanga ni waandishi wa habari pekee waliopo katika Wilaya hiyo na kifo chao kinaweza kusababisha kutoripotiwa kwa matukio mengi katika Wilaya hiyo. Bwana ametoa, na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amen.

Comments