Rais MWINYI wa Zanzibar aanza utekelezaji

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ameutaka uongozi wa Bandari pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuhakikisha kazi za kulitumia ghala jipya la mizigo lililopo Saateni zinaaza mara moja ili kupunguza mlundikano wa makontena katika bandari ya Malindi. Dk. Hussein aliyasema hayo leo huko Saateni mjini Zanzibar mara baada ya kutembelea ghala jipya la mizigo lililojengwa na Kampuni ya Serikali. Katika maelezo yake Dk. Hussein alisisitiza haja ya kutumika haraka ghala hilo kwani hatua hiyo itapunguza mlundikano wa makontena katika bandari ya Malindi huku akikemea tabia ya kufanya kazi kwa mazoea kutokana na Kampuni hiyo ya ujenzi kuchukua muda mrefu wa ukamilishaji wa ghala hilo.

Comments