MBIO ZA UCHAGUZI MAREKANI ZAZIDI KUPAMBA MOTO

Rais Donald Trump amesema kuwa kundi la mrengo wa kulia linastahili kutulia na kuacha sheria kufanyakazi baada ya kukataa kulishutumu moja kwa moja katika mdahalo wa wagombea urais ulioendeshwa kupitia televisheni na kusababisha gumzo. Bwana Trump amesema "Sijui Proud Boys ni kina nani", siku moja baada ya kusema kwenye mdahalo na mpinzani wake Joe Biden anataka kundi hilo "kukaa kando na kuwa tayari". Wanachama wa kundi la Proud Boys wamesema matamshi yake ni kihistoria na ameliidhinisha. Bwana Biden alisema Bwana Trump alikuwa "amekataa kukana kundi la wazungu". Mabadilishano hayo yaliwadia wakati wa mjadala wa kwanza wa mahojiano ya kwenye televisheni kati ya wawili hao kabla ya uchaguzi wa Novemba 3. Mdahalo huo ulibadilika na kuwa mabishano, ugomvi na matusi huku vyombo vya habari vya Marekani vikiuelezea kama vurugu tupu na mbaya usio kifani. Tume inayodhibiti midahalo imesema itaanzisha hatua mpya katika mdahalo utakaofuata kuhakakisha kunakuwa na mwelekeo.

Comments