MAFANIKIO MENGINE NI YA TABU LAKINI MWISHO WA SIKU NI RAHA TU!!!!

Janet Johnson and Michael Brown ni wazazi wenye furaha duniani baada ya kufanikiwa kumpata mtoto wa kiume mwenye afya! Ujio wa mtoto huyo umeushtua ulimwengu kwani ni uzazi unaoweka rekodi kubwa duniani kwa sababu ya kilo nyingi alizo zaliwa nazo huyo mtoto.
Mtoto huyo aliyepewa jina la JaMichael Brown, amezaliwa akiwa na pound 16-sawa na kilo saba na nusu hivi!!

Mama mtoto amesema madaktari walidhani angejifungua mtoto mwenye pound 12 au 13 kutokana na ukubwa wa mtoto waliouona kabla ya kuzaliwa.
Kitaalamu, kilo kama hizo ni sawa na za mtoto mwenye miezi sita tangu kuzaliwa!!

Nawapa hongera kwa kweli, na Mungu awakuzie!!

Comments

Popular Posts