USITHUBUTU KUFUNGUA MLANGO AU GETI LAKO USIKU WA MANANE ETI POLISI WAMEKUJA, WANATAKA WAINGIE!!

UNAWEZA SHANGAA LAKINI NI KWELI IMETOKEA...Kuna Bwana mmoja hivi HUMOUD ISSA HUMOUD wa hapahapa Dar,yeye na familia yake wamejikuta katika tafrani na kulazimika kuyakimbia makazi yao baada ya kuvamiwa na watu waliojitambulisha kuwa ni polisi majira ya saa Nane usiku jana. Huyo bwana amesema akiwa amelala ndani na familia yake alisikia watu wakigonga mlango kwa nguvu na kujitambulisha kuwa ni polisi wakimtaka atoke nje ili wafanye naye mazungumzo ambapo hakuweza kutoka kwa kuhofia usalama wake kutokana na kuwa muda huo ilikuwa ni usiku wa manane. Mbali na kugoma kuwafungulia, alifanya mawasiliano na viongozi wa mtaa wake ambao walikana kuwa na taarifa za ujio wa polisi katika eneo lao usiku huo.Baadae wakaamua kukimbia( sijui walihisi mapolisi watarudi tena!!!)Kwa hiyo Mbali na kutegemea ulinzi wa polisi, wananchi wametahadharishwa kutotii tu kila mtu anayejitambulisha kuwa polisi manake mtu kalala, ni usiku wa manane, kaja kufanya nini nyumbani kwa mtu bila taarifa hata ya maandishi au kama kuna kosa mtu amefanya? ZINGATIA...

Comments

Popular Posts