Hatimaye Ujerumani yagundua chanzo cha E.coli

Ni maharagwe yanayochipua!


Maafisa wa Ujerumani wanasema kuwa wanaamini maharagwe yanayokuzwa nchini humo huenda yakawa ndio chanzo cha maambukizi ya bakteria hatari ya E.coli.
Tangu bakteria hao wazuke,watu 22 wameuawa na wengine 2000 kulazwa hospitalini.
Wataalam kuhusu maambukizi ya maradhi wamegundua kuwa bakteria wa E.coli walitokea katika shamba moja la mimea inayoota kusini mwa mji wa Hamburg.
Waziri wa kilimo katika jimbo la Lower Saxony, mojawapo ya maeneo yaliyoathirika pakubwa na mlipuko huo, amesema kuwa uchunguzi uliofanywa haukubaini moja kwa moja kwamba bakteria hiyo ilitokea katika maharagwe hayo lakini akaongeza kuwa dalili zote zinaashiria kuwa maharagwe ndio chanzo cha maambukizi na wala sio nyanya na matango kama ilivyokuwa iikidhaniwa.

Comments

Popular Posts