LIPUMBA: NITATATUA CHANGAMOTO ZA WALIMU, NIPENI KURA ZENU
Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba amesema endapo atapewa ridhaa ya kuwa rais kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika October 28 Mwaka huu, atahakikisha anasimamia suala la Elimu ikiwemo utoaji wa mafunzo ya kompyuta na intaneti kwa wanafunzi ili kuendana na ukuaji wa sayansi na teknolojia.
Mgombea huyo ameahidi pia kutatua changamoto zinazowakabili walimu nchini.
Profesa Lipumba ameeleza hayo mapema leo wakati akinadi sera za chama hicho kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Soko kuu mjini Shinyanga.
Comments