LISSU AKWAMA KUFANYA MKUTANO MOSHI MJINI

Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu ameshindwa kufanya mkutano wake uliopangwa kufanyika jioni hii katika uwanja wa Mashujaa mjini Moshi. Sababu za kushindwa kufanyika kwa mkutano huo ni kutokana na kuchelewa kufika uwanjani hapo akitokea wilayani Rombo ambapo alikuwa na mikutano mingine ya kampeni. Aidha msafara wa Lissu uliwasili katika uwanja wa Mashujaa majira ya saa kumi na mbili na dakika thelathini na nane ambapo aliteremka na kuwasalimia wananchi kisha akaaga.

Comments

Popular Posts