MAANDAMANO YA WAISLAMU MCHANA HUU, VURUGU KUBWA ZAZUKA KARIAKOO, KINONDONI, NA MAGOMENI

Maeneo ya Msimbazi hali ni tete
Waislamu jijini Dar es Salaam wameanza maandamano mchana huu kutokea katika misikiti mbalimbali iliyopo katika maeneo yao.
Askari wa jeshi la polisi wametanda kila kona ya jiji la Dar es Salaam ili kuzuia kufanyika kwa maandamano hayo, wakitaka kuachiwa huru kwa baadhi ya waislamu, akiwepo katibu wa jumuiya na taasisi za kiislamu nchini, Sheikh Issa Ponda wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa mbalimbali.
Watu walipokaidi amri ya jeshi la polisi...hali ililazimu kuwa hivi
Huko Kariakoo maduka kadhaa yamefungwa kufuatia vurugu hizo zilizopelekea polisi kuwatawanya waandamanaji kwa mabomu ya machozi.

Comments

Popular Posts