TPI YAKANUSHA KUTENGENEZA ARV FEKI...
Uvumi wa dawa feki za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi ulianza kusambaa kama utani kumbe kweli! Jana serikali ilimsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Bohari kuu ya Dawa nchini(MSD) Bw. Joseph Mgaya kwa kushindwa kuifanyia uchunguzi dawa hiyo aina ya TT-VIR 30. Watu wamekuwa wakijiuliza maswali mengi hasa ikizingatiwa mamlaka ya kutengeneza dawa hizo nchini yako kwa kiwanda kimoja tu cha TPI.
Baada ya tuhuma hizo..Leo TPI nayo imeitisha mkutano wa kulizungumzia swala hilo, wakikanusha kuhusika na utengenezaji wa dawa hizo bandia licha ya kupewa mamlaka pekee ya kutengeneza dawa hizo hapa nchini toka mwaka 2007. Kwa habari zaidi usikose kuangalia Clouds Tv saa moja na nusu usiku!
Hizi ndio za kwao wanazotengeneza original.
Comments