JAMANI BINADAMU!!!!!!!!!! BOKO HARAM WAZIDI KUTEKETEZA WATU....

Hebu vuta picha jinsi xmass inavyokuwa na maandalizi na shamrashamra za hapa na pale! Kwa waenda kanisani ndio siku muhimu kweli ya kuhudhuria! Lakini kila kizuri hakikosi ibilisi wa kukimendea< kama ilivyotokea huko Nigeria tarehe 25 ya xmass ya mwaka huu! Watu zaidi ya 30 waliuwawa katika shambulio la mabomu Jumapili, na jana mamia ya watu wakahudhuria sala ya kuwakumbuka marehemu nchini humo.  Nigeria, kanisa liloshambuliwa

Watu zaidi ya 40 walikufa.
Kikundi cha Kiislamu cha Boko Haram, kimesema kuwa kilifanya mashambulio hayo, huku kukiwa na lawama kutoka kwa kiongozi mkuu wa upinzani, Muhammadu Buhari, anaeishutumu serikali kuwa imechelewa kuanza kushughulikia mashambulio hayo na kwamba Rais Goodluck Jonathan hakusema kitu, hadi mashambulio hayo kuanza kulaaniwa dunia nzima.

Comments

Popular Posts