SABA SABA HIYOOOOOOO...VIINGILIO VYA MWAKA HUU TAYARI VIMEWEKWA MEZANI.
Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania ( TanTrade) imetangaza viingilio vipya vya watu na magari katika maonyesho ya kimataifa ya Dar es salaam, (DITF) yatakayoanza tarehe 28 ya mwezi Juni hadi tarehe 8 mwezi ujao.
Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mdhamini rasmi wa mawasiliano wa maonyesho hayo Vodacom Tanzania, Tantrade imetangaza malipo ya Shilingi elfu 2,500 kwa watu mzima na shillingi 500 kwa watoto kila siku isipokuwa siku maalum ya tarehe 7 ambapo viingiio vitakuwa shilingi 3,000 kwa watu wazima na watoto shilingi 1000.
Kwa watakao hudhuria maonyesho hayo na magari madogo watatakiwa kununua tiketi kwa shilingi 4,000, kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha malipo ya huduma nyingine zikiwemo za kupaki magari kama malori na magari makubwa pamoja na huduma nyingine.
Malipo ya ada binafsi.
1. Kwa siku - watu wazima (siku za kawaida) – 2,500/-
2. Kwa siku- watoto (siku za kawaida) – 500/-
3. Kwa siku – watu wazima (siku ya SabaSaba) – 3,000/-
4. kwa siku – Watoto (siku ya SabaSaba) – 1,000/-
5. malipo kwa kipindi chote cha maonyesho - Beji kwa wahusika wa maonyesho - 20,000/-
6. Beji kwa wahusika wa maonyesho (maeneo) – 3,000/-
Comments