WILLY EDWARD HATUNAYE TENA....
Mhariri wa Jambo leo, Willy Edward Ogunde amefariki dunia mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo.
Willy pamoja na wahariri wengine walikuwa Morogoro ambako walikwenda kuhudhuria mkutano wa masuala ya sensa iliyoandaliwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Majira ya saa sita usiku alimwita dereva wa pikipiki afike kumchukua kwa lengo la kurejea katika hoteli alikokuwa amefikia, na baada ya kutoka nje kama hatua sita hivi kabla ya kuifika pikipiki alianguka.
Ndugu zake walimkimbiza hosipitali lakini walipofika na daktari kumpima, tayari alikwishafariki dunia.
Mke wa marehemu aitwae Rehema akifarijiwa na waombolezaji
Mtoto wa marehemu
Comments