HUKO LONDON KUMEKUCHA..WAKILALA, WAKIAMKA , SHAMRASHAMRA NI MOJA TU..OLYMPIC 2012

Wenzetu wanayaweza mashangwe ya kila aina. Familia ya kifalme imeukaribisha mwenge wa Olimpiki katika Kasri la Buckingham katika siku ambapo umati mkubwa wa watu ulikusanyika mjini London kushuhudia mkondo wa mwisho wa safari ya mwenge huo mjini London.
Baada ya tetesi kuwa Uingereza si chochote katika maandalizi ya michezo hiyo, waziri mkuu wao David Cameron amesema michezo ya mwaka huu itathibitisha kuwa Uingereza ina uwezo wa kufanya maandalizi kabambe na hawabahatishi.
Michezo ni mingi mno kasoro Golf na Rugby.. Mie macho yangu na Tv yangu tulii.

Comments

Popular Posts