VIFO VINGINE UTAFKIRI MAZINGAOMBWE....
Katika beach moja huko New Jersey kuna mtoto wa miaka 12 na baba yake walianza kuchimba shimo katika mchanga wa hiyo beach. Na kutokana na ripoti iliyotolewa, walichimba shimo refu kweli katika kujifurahisha. Ghafla bila watu kuelewa haraka haraka kilichotokea, wakashangaa tu wamezama kwenye lile shimo, mchanga ukawafunika, juhudi za kuwaokoa zikaanza but mtoto alikuwa akitokwa na damu sana puani, huku baba mtu akiwa hoi, wakakimbizwa hospitalini. The next day, mtoto alifariki, baba akabaki akipatiwa matibabu hospitalini.
Tumejaliwa beach nyingi, wazazi tuwe makini na michezo watoto wetu wanayoililia.
Wakati mwingine unaweza kuja juta wakati mazingira hatarishi uliyaanzisha mwenyewe kama masihara.
Comments