Guardiola: Muda wangu Barcelona umekwisha
Pep Guardiola anasisitiza kuwa muda wake katika klabu ya Barcelona umekwisha baada ya mkufunzi huyo wa Manchester City kuhusishwa na uhamisho wa kurudi katika mabingwa hao wa Uhispania.
Mgombea wa wadhfa wa urais katika klabu ya Barcelona Victor Font amesema kwamba anafikiri kumrudisha Guardiola iwapo atachaguliwa.
Guardiola aliishindia klabu hiyo mataji 14 wakati akiwa mkufunzi wake.
''Kabla ya kuondoka 2012 kama Meneja muda wangu kuifunza Barcelona umekwisha'' , alisema Guardiola.
''Nilihudumu muda wangu katika klabu hiyo. Mkufunzi aliyepo kwa sasa Ronald Koeman yupo na namuheshimu. Ni rafiki wangu mzuri sana . Pengine watu wengine'' .
Guardiola alikuwa akizungumza baada ya timu yake ya Manchester City kuilaza klabu ya Sheffield United 1-0 katika ligi ya Premia.
Ilikuwa mechi ya tatu ya City katika wiki moja baada ya sare na West Ham kufuatiwa na ushindi wa 3-0 dhidi ya Marseille katika kombe la klabu bingwa siku ya Jumanne.
"Tulicheza vyema sana ," aliongeza Guardiola.
"Tulipata kibarua kigumu kuweza kupata goli ikilinganishwa na nafasi tulizotengeneza, mashambulizi 16, manane yakilenga goli, ni mchezo mzuri dhidi ya timu.
"Ni mechi ya tatu katika siku saba , zote zikiwa ugenini , ni mahitaji ya juu . Watu pia wamezungumzia kuhusu."
Comments