LISSU APINGA MATOKEO YA URAIS

Mgombea wa urais kupitia Chama cha upinzani nchini Tanzania, Chadema bwana Tundu Lissu ametangaza kutokubali matokeo ya uchaguzi. Aidha amesema kuwa uchaguzi huu ulianza kuingia dosari mapema katika kuapisha mawakala ambao ndio waangalizi wa uchaguzi kwa niaba ya chama chao. Lissu amewataka watanzania kudai haki yao kwa njia ya demokrasia na sio kwa vurugu yoyote . Lissu amesema Jumuiya za kimataifa pamoja na jumuiya za kikanda ziingilie kati taarifa za matokeo ya uchaguzi wa Tanzania. "EAC, SADC wasitoe taarifa za kuhalalisha uharamia huu. Waseme ukweli. Watanzania waingilie kudai haki yao kwa amani kwa njia ya kidemokrasia,"Tundu Lissu amesema hayo leo katika mkutano na waandishi wa habari.

Comments

Popular Posts