MIAKA MITANO TENA YAENDA KWA MAGUFULI
Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli ametetea nafasi yake baada ya kushinda kwa kishindo Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumatano wiki hii. Magufuli ameshinda kwa
kupata kura 12,516,252 ambayo ni asilimia 84 ya kura zote zilizopigwa. Tundu
Lissu kutoka chama cha upinzani cha Chadema ameshika nafasi ya pili kwa kupata
kura 1,933,271 ya kura zote ziizopigwa. Jumla ya watu 15,91950 walipiga kura
hizo wakati waliojiandikisha kupiga kura walikuwa 29,754,699 kwa mujibu wa Tume
ya taifa ya Uchaguzi (NEC).
Comments