MAMBO YA MUAMMAR GADDAFI BADO MAZITO,MABILIONI YAKE YAENDELEA KUFICHULIWA!!


Mali ya Kanali Gaddafi yafichuliwa katika eneo kulikofichwa mamilioni ya dola mali ya serikali ya Libya baada ya kufichuliwa kwa stakabadhi ya mamlaka ya uwekezaji nchini humo.

Stakabadhi maalum ya mamlaka ya uwekezaji nchini Libya, ambayo imeonekana na shirika la kutetea haki za binadamu la Global Witness, imeonyesha mwishoni mwa mwezi Juni mwaka jana takriban dola milioni 293 fedha za umma zilihifadhiwa kwenye akaunti za matawi tofauti ya benki ya HSBC ya Uingereza, huku nyingine milioni 275 zikiwekwa kwenye akaunti ya hazina maalum ya benki hiyo.
Inaasemekana kiasi kingine cha dola milioni 110 zimewekwa Royal Bank Of Scotland na dola milioni 182 zimebambwa Goldmans Sachs Bank.
Nayo Benki ya Ufaransa Societe General ilipokea dola bilioni 1.8 kutoka kwa mamlaka ya uwekezaji ya Libya, huku benki ya Nomura ya Japan ikiweka kwenye hifadhi yake dola nusu bilioni mali ya serikali ya Libya.
Mali yote hiyo imepigwa tanji baada ya Jumuiya ya Ulaya na Umoja wa Mataifa kutoka amri hiyo.
Kwa habari zaidi, endelea kuperuzi humu blogini!!!

Comments