NJIA RAHISI TANO ZA KUWA MILIONEA!!!

Sidhani kama kuna asiyependa kuwa milionea.wengi wetu tumekuwa na ndoto  ya kufanikisha malengo yetu.Kuna kitu kimoja cha kujiuliza hapo! Tunawezaje kufika hapo? Majibu yake ni mepesi kuliko unavyoweza kuichosha akili yako kwa mawazo.Hizi ni baadhi ya njia tano kuu za kukufikisha kwenye uwanja wa mamilionea!!!


Hizi ni baadhi ya njia tano kuu za kukufikisha kwenye uwanja wa mamilionea!!!


1.Oa mara moja tu.
Njia hii inamwezesha mtu kuwa milionea  kwa kuwa na familia ya watoto wasiozidi watatu,na mke mwenye kuipangilia familia bajeti ya kawaida!
2.Usiishi kwa kutegemea kipato kimoja tu.
Kuoa ama kuolewa, ni kuunganisha pia nguvu kazi kati ya wawili hao. Hata kama mmoja ana kazi na mwingine hana, mnaweza kuunganisha maarifa ya nini cha kufanya ili kuwe na mfumo mwingine wa kipato cha ziada.
3.Chagua kazi au biashara sahihi.
Iwe umeajiriwa au umejiajiri, hakikisha unachokifanya kinakulipa na kutimiza baadi ya ndoto zako, ama zote ikiwezekana, (japo malengo huwa hayaishi.ukimaliza hili,utawaza jingine).
4.Wekeza fedha zako katika samani.
Tunashauriwa kuwekeza katika vitu vyenye thamani kuliko kuzitumia pesa bila mpangilio.Maisha yanabadilika, na huwezi jua ni lini mkondo wako utayumba na kuhitaji njia mbadala ya kukurejesha katika hali ya nyuma uliyokuwa nayo.Kwa kununua mali zenye thamani, itakusaidia kwa kuviuza pale mambo yanapokwama, na kuzitumia kuzalisha vingine na vingine zaidi.
5.Usiishi maisha ya kimilionea.
Unaweza kuishi maisha ya kawaida na kwa muonekano wa kawaida katika macho ya watu,kutakakokusaidia ku-maintain kipato chako vizuri kimatumizi.Kama tunavyojua,ukiishi maisha ya juu,ndivyo mahitaji nayo yanakuwa ya hali ya juu.

Comments