KATI YA MAMA WA NYUMBANI NA MWANAUME ALIYEAJIRIWA NI NANI ANAKULA MLO MZURI KWA SIKU?
Nimekuta watu wanabishana.Wengine wanasema mwanaume anayefanya kazi ndiye anayekula vizuri kwa siku kwa sababu asubuhi akiondoka nyumbani, pengine hajaacha hela ya kutosheleza ya matumizi hasa chakula, lakini yeye akishaingia eneo la kazi atatafuta supu au vitafunio ambavyo si chini ya elfu mbili na mchana atapata chakula labda si chini ya 2500 au 3000, na kinywaji juu! Na bado akitoka kazini atapita kwa washkaji kupata mbili tatu na nyama choma!!
Sasa kuna wengine wakasema mama wa nyumbani ndo anafaidi kwa kuwa ana uwezo wa kuingia jikoni wakati wowote akapika anachotaka na akala.(ila kama vinono vya kukarangiza havipo, anafaidi kweli hapo!!)
Comments