NILIJUA UHABA WA KAZI NI BONGO TU JAMANI..KUMBE NI TATIZO LA DUNIA!!!!!!!!!!!!!!!!!
Kwa mlio na visomo vyenu na mkabahatika kupata kazi msizichezee..ni bora ukacheza na mshahara na sii kazi.
Imagine, ajira mpya milioni themanini zinahitajika katika miaka mitano ijayo ili kurejesha kiwango cha ajira cha kabla ya mdororo wa uchumi wa mwaka 2008. Sio kasheshe hiyo? Shika ulicho nacho vizuri tu kwa kweli. Na kwa ambae u are seeking for it, usikate tamaa utapata tuu japo yaweza chukua muda kidogo!
Ila mpaka ukisikia ILO imeongea juu ya misukosuko ya kijamii juu ya ajira duniani, kiukweli ni hatariiii!! Halafu sii kwamba maofisi yamefungwa, la hasha...wasomi ni wengi nahisi kuliko maofisi yenyewe au kuna waliotangulia kazini kabla wasomi hawajamalizia kusoma, na hawang`oki ng`ooo!! I hope ni wengi wenu katika ku-apply mnakutana na vikwazo kumi kumi!!
Comments