HII NI BAADA YA MGOMO WA WAALIMU AU NDO UTARATIBU??!
Serikali imewatambua na kuwapongeza wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita, wakiwemo wawili ambao wameingia kidato cha tano kutokea shule za kata.
Akitambua mchango wa wanafunzi hao, Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesema michango ya wazazi na walimu ndicho kichocheo kikubwa cha mafanikio hayo, na amewaomba kuendelea kushirikiana na serikali kuwafundisha watoto kwa bidii ili wafanye vizuri katika masomo yao.
Wanafunzi hao waliopata ufaulu wa daraja la kwanza wametoka katika Shule za Sekondari Marian Girls iliyotoa wanafunzi saba, Mzumbe watatu, Feza wawili, Sekondari ya Kibaha wawili, Kilakala mmoja, Sekondari ya Ufundi Ifunda mmoja, Tabora Girls mmoja, Tabora Boys mmoja, Minaki mmoja na Mpwapwa mmoja.
Comments