WAHENGA WALISEMA..UKITAKA UBAYA, DAI CHAKO...

Kufuatia mauaji ya wachimba madini 34, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza kipindi cha maombolezo ya vifo vyao vilivyo sababishwa na polisi, wakati walipokuwa wakiandamana kudai malipo bora zaidi ya kazi.
Bwana Zuma pia ametaka tume ya uchunguzi ya kisheria ichunguze mauaji hayo katika mgodi wa madini meupe yaani PLATINUM eneo la Marikana. Cha kushangaza, wachimba madini wameamriwa kurejea kazini siku ya Jumatatu la sivyo watafukuzwa kazi. Wengi wamesema kumaliza mgomo wao sasa ni sawa na kuwadhalilisha wenzao waliouawa.
Wanasema watarejea kugoma katika eneo la mgodi huo na wataendelea kushinikiza malipo bora zaidi ya kazi.

Comments

Popular Posts