NADIA SIDIKU BUARI..NDIYE ANAYE-RUN GHANA KWA SASA..

Waigizaji wa Ghana ni wengi na wengine huwa hatuwajui tunaona tu ni wa-nigeria! Huyu ni mmojawapo, nadhani ni wengi tumemuona akiigiza filamu tofauti.
Kipaji chake alianza kukionyesha toka akiwa shuleni kwa kuigiza na kucheza ngoma.Hakukata tamaa, akaendelea kusomea mambo hayohayo mpaka akapata degree yake ya kwanza ya sanaa! Watu wamempachika jina la Beyonce wa Ghana, pengine kwa vile mitoko yao inafanana.
Nadia Buari ni mtoto wa Rais wa zamani wa Umoja wa muziki nchini Ghana Bw.Sidiku Buari.
Kwa Nigeria kuna kina Genevieve Nnanji, Omotola, Ini Edo,Tonto Dikeh n.k wanaokimbiza katika uigizaji, lakini kwa waigizaji wa Ghana, Nadia anawabamba zaidi.

Comments

Popular Posts