FAMILIA YA GADDAFI YATOROKEA ALGERIA!!




Hao ni mke na watoto watatu wa kiongozi wa Libya aliye mafichoni Muammar Gaddafi wanaoelezewa kuwa mafichoni huko Algeria!!
Wizara ya mambo ya nje imesema mke wa kanali Gaddafi, Safia, binti yake Ayesha na watoto wa kiume Muhammad na Hannibal waliondoka Libya mapema jana.

Balozi wa Algeria katika Umoja wa Mataifa amesema walipokelewa kwa misingi ya kibinadamu, lakini waasi wa Libya nao wamejitutumua wakisema kuwapa hifadhi familia ya Gaddafi ni kitendo cha uchokozi, na wametaka warudishwe nchini Libya.

Muammar Gaddafi mpaka sasa hajulikani alipo!!


Ni mmoja wa viongozi ninaowazimikia kwa misimamo yao Afrika achilia mbali mapungufu mengine aliyonayo coz kila mtu pia ana mapungufu yake, HAKUNA MKAMILIFU DUNIANI!
Kafanya mengi sana Libya, hata Umoja wa Mataifa ukihangaika kuijenga bado ni kazi kubwa sana na itachukua miaka mingi, na haitoweza kurudi asilimia 100 kama ilivyokuwa!!  Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!!

Comments

Popular Posts