MUAMMAR GADDAFI TAI SHINGONI!!! WAASI WASHEREKEA KUUTEKA MJI MKUU TRIPOLI.

Shamra shamra za usiku kucha za Waasi na  makundi ya watu wenye furaha vimetawala  katika uwanja wa Green Square, ulio katika mji mkuu wa  Libya-Tripoli, huku wakijitangazia ushindi dhidi ya Gaddafi na kuupa uwanja huo jina jingine jipa la Martyr's Square.
Inaripotiwa kuwa waasi wamemkamata mtoto wa Muammar Gaddafi  Seif al-Islam, huku kanali huyo akiahidi kuwa ataendelea kupigana.
Mwendesha mashtaka wa mahakama ya uhalifu wa kivita, Luis Moreno Ocampo, amethibitisha Seif al-Islam, mwanawe Gaddafi, na ambaye alitarajiwa kumrithi baba yake amekamatwa.
Aidha mtoto wa kwanza wa Gaddafi, Mohammed Al -Gaddafi naye amejisalimisha kwa waasi na anazuiliwa huko mjini Tripoli.
Serikali ya Libya imesema takriban wanajeshi elfu 65 watiifu kwa kanali Gaddafi, wamebakia mjini Tripoli lakini ni wachache tu walioonekana wakati waasi walipokuwa wakielekea kuuteka mji huo.
Mapigano yameripotiwa katika maeneo mengine ya mji, huku waasi wakijaribu kushika udhibiti wa jengo ambalo waandishi wa habari wapo.
Inaaminika kuwa bado Kanali Gaddafi ana maelfu ya wafuasi waliojihami, japo ripoti zinaashiria kuwa idadi kubwa wamejisalimisha kwa waasi.
Msemaji wa serikali ya Libya , Moussa Ibrahim, amesema takriban watu 1,300 wameuwawa mjini humo.
Awali Kanali Gaddafi, aliwataka raia kujitokeza na kuukomboa mji wa Tripoli, akiwahimiza  kutorudi nyuma, na kwamba  watapigana hadi kuikomboa nchi yao kuzuia udhibiti.
Gaddafi amewataka raia hao kutokubali  wanyakuzi kuiteka nchi yao, na kwamba atapigana pamoja nao kama nilivyoahidi.



Waasi waliioonekna wakishangilia ushindi dhidi ya Gaddafi!!


Wanawake, watoto na wanaume wamekesha usiku kucha wakishangilia kuuteka mji wa Tripoli!!

Comments

Popular Posts