WANAWAKE HAWA NI NOMA DUNIA NZIMA!!

Kansela wa Ujerumani Bi. Angela Merkel ametajwa kama mwanamke mwenye nguvu kubwa kabisa duniani. Ni kiongozi asiyetiliwa shaka wa Umoja wa Ulaya.


Orodha ya jarida la Forbes ya wanawake wenye nguvu kubwa duniani inatawaliwa na wanasiasa, wafanyabiashara wanawake na viongozi katika sekta ya habari na burudani. Hii ni mara ya tano kwa kansela Merkel kuongoza orodha hiyo.
Huyu ni wa pili. Ni Hillary Clinton, mke wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton. Mwaka 2008 alikaribia kumshinda rais Barack Obama katika uteuzi wa chama cha Democratic katika kuwania urais wa Marekani.

Nafasi ya tatu imeshikiliwa na rais wa kwanza mwanamke wa Brazil, Dilma Rousseff. 


Tanzania hii wanawake wenye nguvu naamini wapo wengi tu!! Kisiasa, kiburudani, kimuziki, kibiashara, n.k. Na kila mmoja ana wa kwake anaeona anastahili!! Si mbaya ukichangia kwa kuwasilisha jina lake na anachokifanya!!

Comments

Popular Posts