MAREHEMU PATRICK MAFISANGO AAGWA LEO DAR ES SALAAM TAYARI KWA SAFARI YA MAZIKO YATAKAYOFANYIKA HUKO CONGO..
Idadi kubwa ya wachezaji wenzake wa karibu kila mmoja wao anaelezea haamini kama ni kweli amefariki ila anajilazimisha kuamini. Wengine kama Haruna Moshi ndio dah! wameshindwa kujizuia kabisa, kila wakati walitokwa na machozi..
Juma Kaseja ambae alikuwa mmoja wa swahiba wa Mafisango nae akatoa heshima za mwisho
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara nae alifika kuiwakilisha serikali katika nyanja ya michezo.
Haruna Moshi na Juma Kaseja nao wataongozana na msafara mzima mpaka Congo kwa ajili ya kumhifadhi mchezaji mwenzao...Mungu ailaze roho ya marehemu Patrick Mafisango mahali pema peponi Amen..
Comment yako itume kulingana na tukio halisi! Ya ajabu ajabu haitoruhusiwa. Weekend njema kwako mdau!!
Comments