PATRICK MUTESA MAFISANGO WA SIMBA SC HATUNAYE TENA....

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, marehemu Patrick alipata ajali maeneo ya TAZARA alipokuwa akiendesha gari na kujaribu kumkwepa mwendesha pikipiki na kwa bahati mbaya gari lake likakosa uelekeo na kuingia mtaroni na kusababisha ajali iliyomwacha na majeraha makubwa na akaaga dunia muda mfupi baadaye. Jana ilitokea kama bahati alizungumza na watu wengiwengi mmojawapo akiwa ni Christian Bella wa Akudo Band akimuuliza kama walikuwa na shoo jana, christian bella akamwambia hawana shoo so akaamua kwenda Maisha Club.. Na haikuwa kawaida yake kuendesha gari kwani huwa anaendeshwa siku zote lakini jana akajikuta tu anataka kuendesha hivyo dereva akamuachia..kweli kifo hakitabiriki jamani dah... Patrick alijiunga kuichezea Simba SC akitokea timu ya Azam FC. Alizaliwa tarehe 9 Machi 1980 mjini Kinshasa, Kongo D.R.C lakini alikuwa raia wa Rwanda.Mwili wake unatarajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Congo... Poleni sana wana Simba, na mashabiki wote kwa ujumla....Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema Amen.

Comments

Popular Posts